WAKAZI CHEKENYA YAPONGEZWA UJENZI WA ZAHANATI






Na Mwandishi Wetu, Kasulu Kigoma
Wakazi wa kijiji cha Chekenya kata ya Kurugongo wamepongezwa kwa ujenzi wa Zahati kubwa na ya kisasa ya kijiji chao ikiwa ni hatua muhimu ya kusogeza huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi.

Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma walipofanya ziara katika kata hiyo iliyokuwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza katika ziara hiyo Afisa Usafi na Udhibiti wa Taka wa halmashauri hiyo, Ndelekwa Vanica aliyemwakilisha Mkurugenzi, Joseph Kashushura ameitaka kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo kuhakikisha inakuwa na taarifa zote muhimu za ujenzi huo tokea wakati unaanza hadi hatua iliyofikiwa hivi sasa.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kurugongo, Edson Hanyuma amesema kuwa alipata wazo la ujenzi wa zahanati hiyo na kuwashirikisha viongozi wa kijiji ili kusogeza huduma za afya  karibu na wananchi.

Post a Comment

0 Comments