WANAFUNZI WA ELIMU YA WATU WAZIMA KIGOMA WAIOMBA SERIKALI KUWAJENGEA MABWENI

Na Glory Enock Paschal, Kigoma

Wanafunzi waliopo katika mfumo wa elimu ya watu wazima wanaosoma katika shue ya Sekondari Mwananchi Manispaa ya Kigoma ujiji wameiomba Serikali kuweka mazingira rafiki hasa mabweni ya kulala ili waweze kuondokana na chamgamoto ambazo zilisababisha kusitisha masomo hapo awali.

Wakizungumza na Kituo hiki mara baada ya shehere za maadhimisho ya siku ya elimu ya watu wazima, wamesema kuwa licha Serikali kuwapa nafasi ya kurudi shuleni kusoma wengi wao wamekuwa wakishindwa kuendeea vizuri kutokana na changamoto za maisha magumu.

Naye mratibu wa Kituo hicho ambaye pia ni mwalimu wa  shule ya Sekondari Mwananchi  Bw. Deogratias Ammy amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo ni vema serikali kuweka mpango wa mabweni kwa wanafunzi ambao wapo nje ya mfumo rasmi wa elimu.

Kwa upande wake Mkufunzi  Mkazi kutoka Taasisi ya Elimu ya watu wazima Samson Mabula amesema baada Serikali kuweka mfumo wa watoto wa kike waliojifungua wakiwa shule umewasaida wengi kujitambua licha ya changamoto za mazingira wanaoishi.

Haya yote yanajiri wakati wa maadhimisho ya elimu ya watu wazima ambapo kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji yamefanyika katika kituo cha shule ya Sekondari Mwananchi ikiwa ni miongoni mwa vituo vinavyotoa elimu ya watu wazima wakiwemo watoto wa kike walioacha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito.

Post a Comment

0 Comments