WANAFUNZI WATAKIWA KUWEKA JUHUDU KATIKA MITIHANI YAO YA KIDATO CHA NNE







Na. Diana Rubanguka,  Kigoma.
Wanafunzi wa Shule Sekondari Rusesa iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameaswa kuweka jitihada za kila namna ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho ya kidato cha nne.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo, Mkurugenzi wa ofisi ya Mawakili ya (MSASA LAW CHAMBER) ambaye pia ni  Kiongozi wa Mawakili  Kanda ya Magharibi ndugu Thomas Msasa wakati wa mahafali ya yaliyofanyika shuleni hapo mapema leo.

Msasa amesema ni jukumu la wazazi kuunga mkono juhudi za walimu ili kuhakikisha ushirikiano huo unaleta matunda ya matokeo mazuri.

"Niwaombe kwa muda huu uliobaki muongeze juhudi za kusoma ili mfaulu lakini pia nasi wazazi ni jukumu letu kuwasimamia  watoto wetu  na  tuunge mkono juhudi za walimu kwa kuwa tunaona namna wanavyojitoa katika ufundishaji, kufanya hivo nikuunga Mkono kazi kubwa anayofanya Mh. Rais Dkt. Samia katika kuboresha elimu Nchini" amesema Wakili Msasa"

Hata hivyo ili kuunga mkono jitihada hizo Msasa amechangia zaidi ya shilingi laki 5 kwa ajili ya kununua vitabu vilivyokuwa vinakosekana shuleni hapo pamoja na mashine ya kuchapisha na kutoa nakala za mitihani shuleni hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Gumbo Kiondo amesema siyo rahisi kumaliza changamoto za shule za kata kwa kuwa zipo nyingi huku akipongeza majitoleo ya Wakili Msasa kwa kuwa shule hiyo haukuwa na mashine hiyo tangu kuanzisha kwake mwaka 2008.

"Sikutegemea kama mgeni rasmi angetoa machine ya kuzalisha mitihani ambayo tumeshindwa kuipata tangu kuanzishwa kwa shule" lakini pia changamoto za shule za kata si rahisi kumalizwa na mtu mmoja kwa kuwa zipo nyingi" amesema Kiondo.

Aidha ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha kila kata ina shule ya Sekondari na kuiomba Serikali kutatua changamoto ya vifaa vya maabara kwa kuwa shule yake ina maabara ya Phizikia na Kemia ambazo hazina vifaa huku maabara moja ya Biolojia ikiwa ndiyo yenye vifaa hivyo kulazimika kuitumia kwa masomo yote ya sayansi. 


Post a Comment

0 Comments