PROF MKENDA AONGOZA TIMU YA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA AFRIKA WA TEKNOLOJIA ZA KILIMO (ACAT) NCHINI KENYA



Na Mwandishi Wetu, Nairobi. Kenya
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameongoza timu ya Serikali ya Tanzania kwenye mkutano wa Teknolojia za Kilimo Afrika (ACAT) ulioanza jumatatu Oktoba 30, nchini Kenya.

Katika Mkutani huo  Waziri Mkenda ameongoza na  Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Balozi Dkt. Benard Yohana Kibesse, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu na watumishi wengine wa Serikali  ambapo ametembelea maonesho mbalimbali ya Teknolojia za kilimo zinazooneshwa nje ya mkutano huo.

“Nimeona maonesho ambayo kimsingi ni kuhusu jinsi Sayansi na Teknolojia inavyoweza kuleta mabadiliko chanya kwenye kilimo pamoja na ukweli huu tumeona pia umuhimu wa kuzingatia usalama na afya kwenye mabadiliko haya na pia kuchukua tahadhari tusipoteze umiliki wa yale tunayogundua, hasa mbegu bora, ili tusiingie kwenye utegemezi utakaotudhoofisha alisema Prof. Mkenda.

Tanzania kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na taasisi zilizo chini yake imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi inawezesha wabunifu kupitia Programu zake mbalimbali ikimwemo Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu ( MAKISATU) ambayo yanafanyika kila mwaka kwa kuhusisha wabunifu mbalimbali kuanzia kwenye ngazi ya  jamii, Shule za Msingi na Sekondari, Vyuo Vya kati, Vikuu pamoja na Taasisi za Utafiti na kuwapatia washindi fedha na mahitaji mengine ili kuwezesha kukuza bunifu zao na kuzibiasharisha.

Mkutano huo unazinduliwa rasmi leo  jumanne 31/10/2023 na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na kuhudhiriwa na mamia ya wadau wa kilimo kutoka mataifa mbalimbali Duniani 

Aidha Mkutano huo wa (ACAT) umeandaliwa na Serikali ya Kenya kupitia Wizara yake ya Kilimo na Maendeleo ya Ufugaji kwa kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia za Kilimo Afrika (AATF).

Post a Comment

0 Comments