WAANDISHI WA HABARI WATAMBULIWA KAMA WANAJESHI RAFIKI




Na Mwandishi Wetu, Iringa

 Jeshi la Polisi mkoani Iringa limesema kuwa linawatambua waandishi wa habari kama wanajeshi rafiki kwa wanajamii.

Hayo yamesemwa na mkaguzi msaidizi wa jeshi la Polisi na mkuu wa Polisi jamii Noah Mwakyoma wakati akichangia mada katika Mdahalo kuhusu ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari ulioandaliwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC) ambapo amebainisha kuwa waandishi wa habari ni kiungo muhimu kati ya jeshi la Polisi na jamii 

Aidha Mwakyoma amesema mwandishi wa habari ni vema kuzingatia usalama wao wanapokuwa katika majukumu yao ya kihabari hususani katika mazingira hatarishi 

"Mwandishi wa habari hata asipokuwepo habari itakuwepo tu na ili habari hiyo iwafikie walengwa ni lazima kuwe na kiungo ambaye ni Mwandishi wa habari hivyo ni lazima mwandishi huyo awe salama" Mwakyoma 

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa  ACP.  Allan Bukumbi amesema jeshi la polisi mkoani humo lipo tayari kushirikiana na Waandishi wa habari katika kuwatumikia wananchi na kuongeza kuwa changamoto ndogo ndogo  kati ya waandishi wa habari na jeshi la polisi hazitajitokeza tena kutokana na mahusiano mazuri yanayoendelea kuimarishwa kupitia majadiliano ya pamoja 

Mdahalo huo umefanyika Novemba 23, 2023 mkoani Iringa.

Post a Comment

0 Comments