WIZARA YA MADINI YAJA NA MKAKATI KABAMBE KUWAANDAA WATANZANIA WENYE USHINDANI








Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Serikali iko mbioni kupitia na kurekebisha mitaala ya elimu kwa Vyuo Vikuu na vya Kati kwa ajili ya kutengeneza wataalam wa kutosha na wenye ushindani mkubwa kuhudumia Sekta ya Madini nchini.

Hayo yalielezwa na Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Ruben Lekashingo, Oktoba 30, 2023, jijini Dodoma, katika mahojiano maalum na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Madini.

Alisema katika kutafsiri Maono 2030, Madini ni Maisha na Utajiri, Wizara ya Madini imeamua kuongeza nguvu katika nyanja ya uboreshaji wa tija kwa watumishi pamoja na watoa huduma katika sekta ya madini.

Kamishna Janet alisema katika kusimamia ushirikishwaji wa Watanzania katika mnyororo mzima wa Sekta ya Madini, Serikali itashirikiana na Kampuni zilizowekeza sekta ya madini hapa nchini ili kujua uhitaji wao kwenye huduma wanazopatiwa na Watanzania katika miradi yao.

“Tunashirikiana na kampuni hizi ili kujua nini wanahitaji, ili tuboreshe mitaala kwenye vyuo vyetu, kuanzia vyuo vikuu hadi vyuo vinavyofundisha wanaotoa huduma, tunataka tuwe na mitaala ya kimataifa ili wakitoka mafunzoni wakatoe huduma stahiki, wapate uzoefu na waelewe kazi kimatendo.” alisema Janet.

Aidha, Kamishna Janet alisisitiza kuwa namna nyingine iliyopangwa ni kuwaangalia Watanzania ambao walifanya kazi hapa nchini na kutoka nje kufanya kazi kama wataalam kwa kupata taarifa zao ili warudi nchini kufanya kazi kwenye kampuni zilizopo kwa lengo la kufundisha Watanzania ujuzi waliojifunza katika nchi tofauti tofauti.

Kamishna Janet aliongeza kuwa lengo la wizara kufikia 2030 ni kuhakikisha huduma stahiki inatolewa kwa maboresho ili kuongeza tija kupitia wataalam wa ndani na nje ya nchi kwa watumishi na wafanyakazi kwenda nje kujifunza au kuleta wataalam kuja kuwafundisha wafanyakazi hapa nchini.

“Kwa kuangalia kazi zilizopo na kuangalia huduma tunayotoa kwa wateja wetu, tunahitaji kutoa huduma kwa kiwango gani katika kila kazi iliyopo kwenye muundo wetu, tuongeze nini.

Post a Comment

0 Comments