DC KIGOMA: FANYENI VIKAO VYA KIFAMILIA KUEPUKA VITENDO VYA UKATILI







Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kalli amezitaka familia za Manispaa ya Kigoma Ujiji kufanya vikao vya Kifamilia katika kutatua changamoto za kimaisha ili kuepuka vitendo vya ukatili.

Ameyasema hayo Leo Desemba 07, 2023 katika maadhimisho ya Siku kumi na sita (16) za  kupinga vitendo vya ukatili kwa Wanawake na Watoto yaliyofanyika Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Amesema ukimya katika familia kunaweza kupelekea vitendo vya ukatili hivyo ni mhimu familia kukaa pamoja katika kutatua matatizo kwa pamoja.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amewataka Wananchi kuhakikisha Watoto wanapatiwa haki ya elimu, kutoa taarifa za Vitendo vya ukatili katika Mamlaka zinazohusika na kuepuka ukatili wa Kiuchumi na ngono kwa Wanawake Wajasiriamali. 

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo wakishirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo BAKAIDS-Kigoma na Kauli Mbiu ya Mwaka  huu ni,  Wekeza: Kuzuia Ukatili wa Kijinsia.
 

Post a Comment

0 Comments