MRADI WA WEZESHA BINTI WAZINDULIWA KIGOMA KUSAIDIA WASICHANA WALIOKATISHA MASOMO







Na Mwandishi Wetu, Kigoma.

Serikali ya Tanzania na Ubelgiji zimezindua mradi wa Wezesha Binti kupitia shirika la maendeleo la Ubelgiji  Enabel mkoani Kigoma ili kusaidia wasichana waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukatili, ukosefu wa kipato na kubeba ujauzito katika umri mdogo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye amesema ujio wa mradi huo utakuwa na manufaa kwa watoto wa kike kwani utasaidia kupunguza ukatili na kuwafanya kufikia ndoto zao.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Enabel Koenraad Goekint amesema wameamua kuleta mradi huo Mkoani Kigoma nchini Tanzania ili kushirikiana na uongozi kuwanusuru watoto wa kike wanaokumbana na changamoto mbalimbli hasa kufanyiwa ukatili na kushindwa kufika ndoto zao.

Nao baadhi ya wadau wa masuala ya ukatili wa kijinsia Mkoa Kigoma akiwemo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kigoma Msafiri Nzunuri wamesema utekelezaji wa mradi huo ni vyema kundi la wanaume nao likafikiwa ili lipatiwe Elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia, kwani kundi hilo limekuwa likilalamikiwa kufanya ukatili huo.




Post a Comment

0 Comments