UTPC YAANZA MAONYESHO YA KAZI ZA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA KLABU 27 TANZANIA








Na Diana Rubanguka,  Dodoma
Muungano wa Klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) umeanza kufanya maonyesho ya kazi za wandishi wa habari kutoka katika Klabu 27 ikiwa ni moja ya mbinu ya kuwapa motisha waandishi na Klabu zao ili kuweza kujiinua kiuchumi na kuepuka utegemezi.

Kauli hiyo imetolewa na Raisi wa UTPC ambapo amesema kwa mara ya kwanza   taasisi ya UTPC imetambua mchango wa wanahabari na kuamua kusimamia maonyesho hayo ambayo yamekuja na mafanikio makubwa kutokana na bunifu zilizoonyeshwa na wanahabari kupitia klabu zao.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya Klabu  hizo Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo amesema, UTPC itayachukua yote  iliyoyaona katika mabanda na kuyasimamia ili kufikia ndoto za kila klabu.

Amesema pamoja na kuwa maonyesho hayo ni ya mara ya kwanza na maandalizi yamefanyika kwa muda mfupi bado maonyesho yamekuwa mazuri na tunatarajia kuwa maonyesho yajayo yatakuja na matokeo chanya.

Kwa upande wake Jane Shussa, Afisa Mwandamizi Mawasiliano ya Kidigitali kutoka TWAWEZA amesema,  Vyombo vya habari vikiwa huru vinaweza kusaidia kutatua migogoro katika jamii, kwa kuwa sekta ya habari ikibadilika italeta mabadiliko katika jamii zetu.

Miradi ya maendeleo inayofanywa na Press Club itakuza taaluma na ni matarajio kuwa miradi ambayo imeonyeshwa, imeonyesha utayari wa kutoka tulipo na kwenda sehemu nzuri zaidi, na kwamba  mabadiliko haya ni makubwa huku akitoa wito  kwa wanahabari kujisemea katika changamoto zao ili kufikia mafanikio tarajiwa ya tasinia yao.

Nae Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya amesema jukumu la UTPC ni kuyachukua na kuyafanyia kazi yaliyoonyeshwa na Klabu zote ili kuhakikisha kila Klabu inafikia mafanikio ya ndoto zake .

Amezipongeza klabu kwa maandalizi makubwa yaliyofanyika na kuja na vitu vikubwa, na kutoa pongezi kwa wafadhili wa UTPC ambao ni ubarozi wa SIDA kwa kuendelea kuwa na UTPC.

Kwa niaba ya viongozi wa Klabu za wanahabari nchini mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Dar es salaam (DPC) Samsoni Kamalamo amesema kupitia maonyesho hayo kuna mengi ya kubeba na kwenda kuyafanyia kazi ili kukua kwa pamoja na kufikia hatua ya kujitegemea na kujikwamua kiuchumi.

"kila mmoja amepata nafasi ya kujifunza ambacho anaweza kuendeleza katika Klabu yake, na hii imeonyesha ni kwa kiasi gani kila mmoja anaweza kujisimamia pekee yake na akuendelea kuhabarisha jamii bila kutegemea ufadhili" Amesema Kamalamo.

Post a Comment

0 Comments