WAANDISHI WA HABARI WAMETAKIWA KIANDIKA HABARI ZENYE TIJA KWA JAMIII.





Na Diana Rubanguka, Kigoma 
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Rais wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) Deogratius  Nsokolo ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuandika habari zenye tija kwa wananchi lengo ikiwa ni kufikisha habari hizo kwa serikali.

Wito huo ameutoa leo ijumaa wakati akifungua mkutano mkuu wa 13 wa kawaida wa wanachama wa KGPC, ambapo amesema waandishi wamekuwa wakishiriki ziara za viongozi na kurudi na habari za ziara hivyo watumie ziara hizo kuandika habari za wananchi kwa kuwa bado wana changamoto nyingi zinazowakabiri.

"sisi ni mashahidi, tukipita mikoa ya wenzetu tunajionea utofauti ulipo kati ya Mkoa wetu na mikoa mingine, tuzisemee hizi taarifa ili kuchochea mabadiliko ya Mkoa wetu" amesema Nsokolo.

Post a Comment

0 Comments