WACHIMBA MADINI KAKONKO WAOMBA KUSOGEZEWA HUDUNA ZA AFYA


Na James Jovin, Kakonko

Wachimbaji wa madini katika eneo la NYAMWIRONGE wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kupeleka huduma za afya, umeme na maji kwenye eneo hilo kurahisisha shughuli za uchimbaji.

Baadhi ya wachimbaji hao Wolta Bernad na Kolimba Paulo wamesema mbali na changamoto hizo wanatumia zana hafifu katika uchimbaji jambo ambalo linakwamisha shughuli hizo sambamba na kulipa kodi kwa mujibu wa sheria

Mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Evance Mallasa akizungumza na wananchi wa eneo la Nyamwironge amesema serikali inaendelea na jitihada za kupeleka huduma muhimu kwenye eneo hilo na kuwasisitiza wachimbaji kulipa kodi sambamba na kuheshimu sheria za ardhi na mazingira kwa ujumla
 
Mkuu wa mkoa wa Kigoma kamishna wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye pamoja na kusisitiza huduma kupelekwa nyamwironge haraka iwezekananvyo amewataka wachimbaji kulinda afya zao sambamba na usalama ili wafanye kazi zao katika mazingira mazuri

Post a Comment

0 Comments