WANANCHI WAMETAKIWA KUTOKUWA CHANZO CHA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

 


Na Mwajabu Hoza , Kigoma.

MKUU wa wilaya ya Kaulu Kanal Isack Mwakisu amewataka wananchi kuacha tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya uhifadhi wa vyanzo vya maji ili kuendelea kutunza uoto wa asili pamoja na kutumia vyanzo hivyo kubuni miradi ambayo itawaingizia kipato.

 

Akimwakilisha mkuu huyo wa wilaya Katibu Tawala Theresia Mtewele amesema hayo wakati wa uhamasishaji wa wananchi kupokea mradi wa upandaji miti katika bwawa la Kamve lililopo kijiji cha Kumtundu wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma mradi ambao unatekelezwa na serikali kupitia wakala wa huduma za misitu TFS kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

 

Amesema uharibifu wa maeneo ya vyanzo vya maji ikiwemo eneo la bwawa la Kamve uliofanywa na wananchi kwa shughuli za kilimo na uvuvi usio rasmi umechangia kupungua kwa kina cha maji na hivyo kusababisha  hata uwekezaji katika bwawa hilo kuwa mgumu kutokana na wakulima kulima pembezoni mwa bwawa hilo.

 

Amesema nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo wananchi wanapaswa kuzingatia sheria hizo katika usimamizi wa hifadhi za vyanzo vya mito na hivyo kuwataka wananchi kushirikiana na serikali kulinda maeneo hayo ya hifadhi na atakayekiuka sheria zitachukuliwa dhidi yake.

 

“Nimeambiwa katika bwawa la Kamve kuna samaki wapo na wavuvi wamekuwa wakivua kawaidia na hivyo kuadhiri samaki zilizomo ambazo zinaendelea kukuwa hivyo namtaka kaimu mkurugenzi Amidius kuhakikisha ndani ya siku kumi na nne wanashirikiana na uongozi wa kijiji kuandaa andiko litaonyesha namna gani uvuvi wa kisasa unaweza kufanyika katika bwawa” Amesema  

 

Mtewele amesema ni wakati wa wananchi kupokea mradi wa upandaji miti ambao utasaidia kutunza mazingira katika bwawa hilo ili hata wafadhili mbalimbali waweze kuendelea kuwekeza katika Nyanja mbalimbali lakini pia serikali inaweza kutumia mapato yake kuwekeza kwenye bwawa hilo ili kijiji kiweze kupata mradi wa kujiingizia kipato.

 

Juma Stunda na Lucas Jonasi wamesema ili waweze kunufaika ipasavyo na uvuvi wa kisasa wanahitaji elimu ambayo itawasaidia wao kuweza kumudu kuvua kisasa na kuachana na uvuvi wa kawaidia ambao umekuwa ukiathiri mazalia lakini pia kuacha kulima kilimo pembezoni mwa bwawa hilo na kuadhiri uoto wake wa asili na kupungua kwa kina cha maji.

 

Wamesema wao wapo tayari kupokea mradi wa upandaji miti ya kuitunza na hivyo kuwaomba viongozi wa kijiji nao wawe tayari kuupokea maana wao ndio wamekuwa chanzo cha kukaribisha mifungo katika maeneo yao ambayo inaaenda kuharibu vyanzo vya maji.

 

Mwakilishi wa  meneja wa RUWASA wilaya ya Kasulu amesema walipotembelea eneo lote la bwawa hilo wamebaini kuwa ni chanzo kizuri ambacho wanaweza kukitumia kuanzisha mradi wa maji ambao utawasaidia wananchi wa kijiji hicho cha Kumtundu na vijiji jirani.

 

Kaim afisa misitu wilaya ya Kasulu Dorisia Kasula amesema lengo lao kwa kushirikiana na UNHCR ambao ndio wafadhili wakuu wa miche laki 250 ambayo wanatarajia kuipanda katika bwawa hilo wanataka kuhakikisha wanarudisha uoto wa asili ambao umepotea kwenye bwawa hilo.

 

Amesema wamekagua na kuona uharibifu mkubwa unaotokana na shughuli za kilimo ambao utaadhiri faida ambazo zinaweza kupotea endapo hatua za haraka hazitachukuliwa ambapo bwawa hilo ndilo linalotumika kupeleka maji yake katika Ziwa Tanganyika.

 

Vijiji ambavyo vitanufaika na mradi huo wa vitalu vya upandaji miti katika wilaya ya Kasulu ni pamoja na vya Kumtundu, Kalimgomba, Mvugwe na Kumkombati ambapo mradi huo umegharimu kiasi cha milioni 200 katika hatua ya upandaji wa vitalu vya miti

 

Post a Comment

0 Comments