AHUKUMIWA MIAKA 30 JERA KWA KUBAKA BINTI WA MIAKA 15.


Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
Mahakama ya Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma imemuhukumu mshitakiwa Kwizera Nyakubusa (20) mkulima na mkazi wa Kitahana wilayani Kibondo kwenda jela miaka 30 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye miaka 15.

Mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 28,2023 huko Kijiji cha Kitahana wilayani Kibondo Mkoani Kigoma na alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Oktoba 30,2023.

Akitoa hukumu hiyo Januari 11,2024 hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kibondo mheshimiwa Maila Makonya amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria, maadili na ukatili dhidi ya watoto.

Post a Comment

0 Comments