JAMII KIGOMA YASHAURIWA KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE UHITAJI






Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
Jamii mkoani Kigoma imeshauriwa kuwakumbuka watu wenye uhitaji kwa kuwa nao wanayo haki ya kupata mahitaji muhimu ya binadamu.

Wito huo umetolewa na 
Mkurugenzi Mtendaji wa Msasa Law Chamber wakili Eliutha Kivyiro taasisi hiyo ilipotembelea kituo cha kulelea watoto wasio na walezi  cha MWOKACHI kilichopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.

Kivyiro amesema, kila mtoto anayo haki ya kupata mahitaji muhimu na katika kuunga mkono juhudi za kituo hicho, Msasa Law Chamber imetembea kituo kicho na kutoa sadaka kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii kwa kuwa wamekua walifanya kazi na jamii.

Wakili Kivyiro Alitoa pongeza kwa mkurugenzi wa kituo hicho kwa kuchukua jukumu la malezi kwa watoto ambao wangeweza kuwa watoto wa mtaani kwa kuwa mtaani kuna watoto wengi ambao wengi wao hawana wazazi wala walezi.

Akizungumza kituoni hapo wakili 
Prosper Magaibuni,  amesema ni changamoto kulea mtoto ambaye siyo wa kwako kwa kuwa kila mmoja ametokea mazingira yake, na kuongeza kuwa malezi yanayotolewa ni sadaka ambayo mwenyezi Mungu ataiongezea, kwa kuwa uwepo wa watoto hawa kituoni unapunguza wimbi la watoto mtaani.

"Siyo kazi rahisi kulea mtoto ambaye haujamzaa kwa kuwa kila mmoja ametoka kwao na tabia yake, lakini mmeweza kuwakusanya na kuwalea katika misingi  bora ya malezi" amesema kivyiro.

Kwa upande wake afisa  maendeleo ya jamii kituoni hapo Rabani Amos amesema, kituo kina watoto 156 ambapo 75 wanalelewa hapo huku 92 wakipatiwa mahitaji muhimu wakiwa kwa ndugu zao.

Awali watoto wote 156 walikuwa wanalelewa kituoni hapo lakini kutokana na changamoto za chakula kituo kililazimika kupunguza watoto wenye ndugu mtaani ili wahudumiwe wakiwa nje.

Post a Comment

0 Comments