JESHI LA POLISI LAKAMATA SILAHA 16 MKOANI KIGOMA


Na Mwanidhi Wetu, Kigoma
Jeshi la Polisi mkoani kigoma limefanikiwa kukamata silaha 16  zilizokuwa  zinamilikiwa kinyume na sheria huku  zaidi ya washtakiwa wawili wa kesi hiyo wakihukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki silaha aina ya gobore kinyume na sheria.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Philmon Makungu ametoa taarifa hiyo hii leo January 15 ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Katika hatua nyingine Kamanda makungu amesema katika kuzuia ajali za barababarani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari  hadi Disemba 2023 jumla ya makosa 62,917 ya usalama barabarani yamekamatwa na kutozwa faini.

Ameongeza kuwa, kwa upande wa dawa za kulevya Mahakama ya wilaya ya kasulu imemhukumu kifungo cha kwenda jela kwa miaka 50 mshtakiwa mmoja wa kesi ya kulima dawa za kulevya aina ya bangi.

Hata hivyo jeshi la polisi limewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kuzuia na kubaini uhalifu na wahalifu kwa lengo la kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Post a Comment

0 Comments