UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI WAFIKIA ASILIMIA 84 KWA MWAKA 2023


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Hali ya upatikanaji wa dawa muhimu na bidhaa nyingine za Afya (aina 290) katika vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma vimeongezeka kufikia 84% mwaka 2023 kutoka 58% Mwaka 2022. 

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo Januari 10, 2024 wakati akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za Afya nchini kwa mwaka 2023 wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam.

Waziri Ummy Mwalimu amesema hali ya upatikanaji wa bidhaa za Afya mwaka 2023 kwa ngazi za Zahanati ikiwa ni 75%, Vituo vya afya 69%, Hospitali za Wilaya 82%, Hospitali za Rufaa za Mikoa 93% pamoja na Hospitali za Taifa na Kanda Maalum 99%. 
 
“Upatikanaji wa dawa katika ngazi ya msingi umeongezeka ambao ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, sasa ni wajibu wetu kuhakikisha vituo vyote vinapata bidhaa za dawa muhimu zote.” Amesema Waziri Ummy

Post a Comment

0 Comments