ZINGATIA HAYA KUJIKINGA NA UGONJWA WA MACHO MEKUNDU



Kuhusu Ugonjwa maambukizi ya ngozi ya juu ya gololi la jicho (Viral Conjuctivitis) maarufu kama red eyes 👀👀

Zingatia haya ujikinge:

➡️Usiguse guse macho; maambukizi hutoka kwenye viganja vya mikono kuja kwenye macho
➡️ Nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni

➡️Wakuu vitakasa mikono muhimu sana kipindi kama hiki

➡️Usichangie vipodozi na vitu vingine unavyotumia  kama vile wanja, tishu, nguo au dawa za macho nk

➡️ Usishike mikono watu hovyo, iwapo umeshika takasa mikono

Pia zingatia yafuatayo:

➡️Kutokutumia dawa zisizo rasmi na ambazo  hazijaandikwa na daktari.

➡️Usitumie dawa za macho anazotumia mgonjwa  mwingine au alizoandikiwa yeye awali alipokuwa na tatizo la jicho ili  kuepuka madhara.

Post a Comment

0 Comments