JELA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 9


Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mahakama ya Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imemuhukumu mshitakiwa Moses Method (23), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kasuga wilayani Kakonko kwenda jela maisha na kulipa fidia kwa muhanga ya fedha taslimu Tsh.1,000,000 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili(9).

Mshitakiwa ametenda kosa hilo Agosti 17,2023 huko  Kijiji cha Kasuga Wilayani humo na alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 21,2023.

Akitoa hukumu hiyo Februari 12, 2024 hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kakonko mheshimiwa Ambilikile Kyamba amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria, maadili na ukatili dhidi ya watoto.

Post a Comment

0 Comments