JESHI LA POLISI KIGOMA KUNDELEZA MAHUSIANO NA WAANDISHI WA HABARI

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi SACP Filemon Makungu (Kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma (KGPC) ambaye pia ni Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo baada ya mazungumzo.

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Jeshi la polisi mkoani Kigoma limesema litaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati yake na Waandishi wa Habari mkoani humo kupitia jukwaa la ulinzi na usalama wa waandishi pamoja na kuzingatia uboreshaji wa kazi.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi SACP Filemon Makungu amezungumza hayo ofisini kwake wakati wa mazungumzo na Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma (KGPC) ambaye pia ni Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo.

Kamanda SACP Makungu amesema Polisi inawatemea waandishi katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo kufikisha habari kuhusu utendaji kazi wa jeshi hilo na elimu mbalimbali kwa jamii.

Kwa upande wake Deogratius Nsokolo wa klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma (KGPC) ambaye pia ni Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), amesema ushirikiano uliopo kati ya jeshi la polisi na waandishi wa habari unarahisisha kazi kwa pande zote mbili.

"Jeshi la polisi linawaitaji waandishi wa habari ili wayaseme yale yanayofanywa na jeshi hilo wakati waandishi wanalihitaji jeshi la polisi kukamilisha kazi yao ya kuhabarisha jamii pia hata suala la usalama kwa waandishi, hivyo kutunza uhusiano wetu ni jambo la msingi kwa kila upande" amesema Nsokolo.

Aidha Nsokolo ametumia nafasi hiyo kumpongeza SACP Makungu kwa kupandishwa cheo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan ambaye ndie Amiri Jeshi Mkuu.

Ikumbukwe kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Filemon Makungu kabla ya Cheo hicho alikuwa na cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP.

Post a Comment

0 Comments