KIGOMA YAJIPANGA KUDHIBITI URASIMU MAUZO YA MADINI


Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Serikali mkoani Kigoma imejipanga kukabiliana na kudhibiti  biashara haramu ya madini na vito vya Thamani kwa kufungua Jengo jipya ambalo biashara hizo zitafanyika kwa kuzingatia kanuni na taratibu za serikali. 

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameyasema hayo alipozungumza kwemye hafla fupi ya kufungua jengo hilo lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji leo, februari 20, 2024. 

Jengo hili litaziba mianya ya utoroshwaji  wa Madini, ukwepaji kodi sambamba na uchakataji holela wa madini jambo linaloipa serikali na wafanyabiashara hasara kubwa.

Amezitaja huduma zitakazotolewa kupitia jengo hilo kuwa ni ukaguzi wa madini na vibali, ununuzi na uuzaji wa madini, utozaji wa mirabaha,  uhifadhi wa madini, utoaji wa vibali vya kusafirisha madini, uendeshaji wa minada ya vito sambamba na uchakataji mdogo wa madini. 

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wafanyabishara wa madini ndani na nje ya mkoa kuzingatia matumizi ya soko hilo sambamba na kufuata sheria za uuzaji, unununzi na uhifadho wa madini.

Post a Comment

0 Comments