JAMII YAONYWA KUMALIZA VITENDO VYA UKATILI NJE YA MAHAKAMA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh Thobias Andengenye (Mwenye suti nyeusi) akipokea dumu la mafuta kutoka kwa mjasiliamali mwanamke katika maazimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kijiji cha makele wilayani Kasulu.



Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Jamii mkoani hapa imetakiwa kuachana na tabia ya kumaliza mashauri  yanayohusu ukatili wa kijinsia nje ya mifumo ya kisheria na kusababisha usugu wa vitendo hiyo. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipozungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku wa wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika kata ya Makere wilayani Kasulu. 

"Tafiti zinaonesha kuwa Asilimia Sitini (60) ya matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hufanywa katika gazi ya familia huku kukiwa hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa na kusababisha usugu wa tabia zinosababisha vitndo hivyo  vyenye kuketa athari na maumivu ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii" amesema Andengenye. 

Aidha katika  kufikia kasi ya mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kundi hilo mkoani Kigoma, Mkuu huyo wa mkoa amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri kuimarisha uratibu na  usimamizi wa shughuli za kielimu, hamasa kuhusu uwekezaji  na masuala ya usawa wa kijinsia kwa lengo la kuleta ustawi wa jamii. 

Pia Andengenye amewaelekeza watendaji hao kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbli wa maendeleo katika kutekeleza mpangokazi wa Taifa wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku akiitaka jamii kutoendelea kufumbia macho vitendo hivyo kwani vina athari kubwa kwa watendewa. 

Kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi, Andengenye amekumbusha wanawake mkoani hapa kutumia fursa za maboresho makubwa ya miundombinu ya uchukuzi na Nishati ya Umeme, ili kujiletea maendeleo na Taifa kwa ujumla. 

Kadhakika katika kuimarisha mfumo wa utawala bora, mkuu huyo wa Mkoa amewaasa wanawake mkoani hapa kushiriki chaguzi mbalimbali kwa lengo kugombea nafasi za uongozi ili waweze kupata fursa ya kuonesha umahiri wao katika ngazi  mbalimbali za kiutawala.

Post a Comment

0 Comments