KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YAPITISHA MAPENDEKEZO YA BAJETI YA WIZARA YA AFYA




Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Stanslaus Nyongo imepitisha makadirio ya Mpango wa mapato, Matumizi ya kawaida na Miradi ya Maendeleo Shilingi trilioni 1.34 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 1.23 mwaka 2023/2024 ikiwa na sawa na ongezeko la asilimia 8.9.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameishukuru Kamati hiyo kwa kupitisha mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Afya na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha zitakazotumika kuboresha sekta ya afya na kufikisha huduma bora za afya karibu na wananchi.

"Katika mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara na Hospitali zilizo chini yake inakadiria kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 756.86 sawa na ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na bajeti ya makusanyo ya maduhuli ya mwaka 2023/24. Kati ya fedha hizo, Shilingi milioni 70.82 zinatarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya Makao Makuu ya Wizara na Shilingi milioni 134.17 kutoka Hospitali za Rufaa za Mikoa na kiasi cha Shilingi milioni 551.86 kutoka Taasisi, Hospitali ya Taifa, Maalum na Kanda". Amesema Waziri Ummy.

Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 iliyowasilihswa katika Kamati hiyo imeweka imebainisha matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo, ambapo imebainisha Shilingi milioni 631 zitatumika katika matumizi ya kawaida ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 25 kutoka shilingi milioni 502 zilizotengwa mwaka 2023/24 huku shilingi milioni 715.2 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwa ni pungufu ya asilimia 2.3 kutoka shilingi milioni 732.3 zilizotengwa mwaka 2023/24.

Aidha, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuandaa bajeti inayolenga kuboresha ubora wa huduma za afya nchini pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kufikisha huduma bora kwa wananchi katika maeneo yao.

Post a Comment

0 Comments