MKUU WA MKOA KIGOMA AITAKA JAMII KUACHA KUKATA MITI YA ASILI




Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameitaka jamii kuacha kukata miti ya asili huku akisisitiza upandaji wa miti yenye tija ikiwemo ile ya matunda

Mh Andengenye ameyasema hayo aliposhiriki kampeni ya mti wa mama inayohusisha upandaji wa miti kama sehemu kuhamisisha uhifadhi wa mazingira.

Kampeni hiyo ambayo hufanyika tarehe 27 ya kila mwezi ikiwa ni katika kuadhimisha kumbukumbu ya tarehe ya kuzaliwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  na hamasa yake katika utunzaji wa Mazingira.

Zoezi hilo limefanyika katika Shule ya Sekondari Katubuka iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuhudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa, Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kalli,  Wakuu wa Idara na Sehemu katika Sekretariet ya Mkoa, Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mganwa Nzota, Afisa Tarafa Kigoma Kaskazini Maximilian Ngasa pamoja na watendaji wengine wa serikali .

Post a Comment

0 Comments