RAIS DKT. SAMIA ATOA TAKRIBANI TSH TRILIONI 11 KUONDOA CHANGAMOTO MKOANI KIGOMA





Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye amesema mkoa wa Kigoma katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeshapokea shilingi trilioni 11.450 ili kuondoa changamoto zilizofanya mkoa wa Kigoma kuonekana kati ya mikoa yenye changamoto nyingi kimaendeleo.

Mh. Andegenye ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Makere wilayani Kasulu.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa, uongozi wa Rais Dkt. Samia umeakisi uwezo na umahiri walionao wanawake katika kuiendeleza duniani.

"Ni dhairi kwa sasa tunatembea kifua mbele kwasababu tunajua dunia imetupia macho Tanzania ikijifunza namna Rais wetu alivyoweza kutuvusha ambapo tunaiongelea nchi yetu bila aibu tukiwa vifua mbele,” amesema Mkuu wa mkoa Andengenye.

Post a Comment

0 Comments