UONGOZI KIGOMA PRESS CLUB (KGPC) WAMTEMBELEA RC KIGOMA MH. ANDENGENYE








Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma (KGPC) Deogratius Nsokolo akiwa na Ujumbe wake leo Aprili 25, 2024 amemtembekea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ofisini kwake na kufanya mazungumzo mafupi kuhusiana na maendeleo ya Tasnia hiyo mkoani hapa.

Kupitia mazungumzo yao, wawili hao wamekubaliana kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha jamii ya wanakigoma na watanzania kwa ujumla wanaendelea kupata taarifa mbalimbali ikiwemo zile za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kazi mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema tasnia hiyo ni nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa mkoa, kuhamasisha amani, ushirikiano, pamoja na kuifanya jamii kupata habari mpya kuhusu masulala mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa wa Kigoma.

Post a Comment

0 Comments