TRA WAKAMATA POMBE, VIPODOZI VYA MAGENDO KIGOMA




Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MAMLAKA ya mapato TRA mkoa Kigoma imekamata bidhaa mbalimbali za pombe na vipodozi ambavyo thamani yake haujatambulika hadi sasa vikiingizwa nchini kwa kutumia njia zisizo halali na  kukwepa kulipa kodi huku wenye bidhaa  hizo wakizitelekeza na kukimbia 
 
MeneJa wa TRA mkoa Kigoma, Deogratius Shuma  akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari kwenye kituo cha forodha cha Mamlaka hiyo eneo la Manyovu wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma alisema kuwa bidhaa hizo zimeingizwa  kupitia vijiji vilivyopo mpakani mwa Tanzania na Burundi katika wilaya ya Buhigwe.
 
Alivitaja bidhaa hizo kuwa ni Pamoja na pombe kali aina ya Karibu  Waragi Gin katoni 95, Dubai Gin katoni tano,kinyaji cha kuongeza nguvu aina ya akayabagu Katoni  nane, vipodozi vilivyopigwa marufuku katoni 106.
 
Katika operesheni hiyo pia wamekamata  mifuko 15 ya vipodozi ya kilo 25 kila moja aina ya Altar Marine Blue ambavyo pia vinatumika kama kemikali ya kutengenezea sabuni na sigara aina ya club ambazo zimeingizwa bila kufuata taratibu zakulipiwa ushuru.
 
Sambamba na hilo Meneja huyo wa TRA mkoa Kigoma amesema kuwa Pamoja na kukamatwa kwa bidhaa hizo ambazo wamiliki wake wamekimbia pia wanayashikilia magari mawili aina ya Toyota Probox na pikipiki moja vilivyokamatwa vikisafirisha mzigo huo.
Baadhi ua wananchi wa wilaya ya Buhigwe wakiongea na waandishi wa Habari walisema kuwa uingizaji bidhaa kwa njia ya magendo kuna athari kwa nchi kwani unaifanya serikali kushindwa kukusanya mapato ya kutosha ambayo ndiyo yanayosaidia kugharamia miradi ya wanchi.
 
Mmoja wa wananchi wa mkoani Kigoma  Juma Majaliwa mkazi wa Kijiji cha Mnanila wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma alisema kuwa uingizaji nchini bidhaa kwa magendo bila kulipia ushuru unainyima serikali mapato kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba vijiji vya mpakani wilayani humo vimeshamiri kwa vitendo hivyo.

Post a Comment

0 Comments