HALMASHAURI ZATAKIWA KUONGEZA UFANISI MAKUSANYO YA NDANI





Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Halmashauri za mkoa Kigoma zimetakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vyanzo vilivyopo ili kuziwesesha halmashauri kukusanya mapato ya kutosha yatakayoweza kugharamia mipango yake ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya ndani.
 
Mwenyekiti wa Mamlaka ya serikali za mitaa (ALAT) mkoa Kigoma, Jackson Mateso alisema hayo katika kikao cha kawaida cha mamalaka hiyo kilichofanyika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma na kueleza kuwa halmashauri kukusanya mapato ya ndani ya kutosha kunachochea miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa kiasi kikubwa.
 
Mateso alisema kuwa hiyo ni azimio la kikao cha ALAT kwa wakurugenzi wa halmashauri kuona namna wanavyofungua macho na mawazo katika kuangalua namna gani wanaongeza mapato kutoka kwenye vyanzo mbalimbali lakini pia kwenye vyanzo vilivyo ni lazima wahakikishe vinasimamia vizuri na mapato ya kutosha yanakusanywa.
 
Akizungumzia azimio hilo la ALAT Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kasulu,Dk. Semistatus Mashimba alisema kimsingi azimio hilo la ALAT mkoa linatokana na mchango wa wajumbe wa kikao hicho kutokana na maadiliano yanayoonyesha baadhi ya miradi inayotekelezwa kwa mapato ya ndani kuchukua muda mrefu kukamilika kwa kukosa fedha hivyo suluhisho limeonekana halmashauri zisimamie kwa karibu kuona mapato yanaongezeka.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kakonko, Ndaki Stephano alisema kuwa kilimo ni moja ya maeneo yenye tija kubwa katika kuongeza mapato ya halmashauri hivyo ametoa ushauri kwa wakurugenzi wenzake Kwenda kuangalia upya chanzo hicho na namna kinavyoweza kuchangia mapato makubwa ya halmashauri kupitia maakusanyo ya ndani.
 

Post a Comment

0 Comments