MAASKOFU WA MAJIMBO WAPONGEZWA






Diana Rubanguka, Kigoma.
Askofu wa jimbo katoriki Kigoma Joseph Mlola, amewapongeza maaskofu kutoka majimbo matatu kwa heshima walioionyesha kwa waamini wa jimbo katoriki Kigoma kwa kuwasindikiza Maaskofu mkoani Kigoma akiwemo Mwadhama Protase kadinari Rugambwa na Muhashamu askofu mstaafu Paul Ruzoka wa jimbo la Tabora waliotembelea mkoa huo kwa lengo la kushukuru.  

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa mapokezi ya kuwapokea Maaskofu hao Mwadhama Protase kadinari Rugambwa Askofu Jimbo kuu la Tabora na Muhashamu akofu mstaafu Paul Ruzoka wa jimbo la Tabora wakati walipotembelea jimbo la Kigoma kwa ajili ya shukrani kwa jimbo hilo ambalo ni jimbo mama kwao.

“tunamshuru sana mwenyezi Mungu kwa kuwafikisha salama wageni wetu hapa nyumbani kigoma, tumpe Mungu sifa na utukufu, wageni wetu kutoka Jimbo la Tabora hongereni na poleni kwa safari hiyo ndefu, asanteni kwa heshima mliyoionyesha na karibuni jimboni kwetu na asanteni sana nanyi nyote kutoka huko Kahama na Mpanda” amesema Askofu Mlola.

Akizungumza baada ya mapokezi hayo kwa niaba ya wageni wote alioambatana nao kutoka jimbo kuu la Tabora,  Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa amewashukuru waamini wa Kanisa Katoeriki Kigoma kwa mapokezi Mazuri na kusema kuwa ni matarajio yake kuwa wataendelea kuwa pamoja katika mambo mbalimbali ya kiwemo ya kiroho.

Naye makamu wa askofu wa Jimbo Katoriki Kigoma Padre Evarist Guzuye, amesema kuwa wanayo furaha kubwa mioyoni mwao kuwakaribisha viongozi  hao na wote walioambatana nao kwa lengo la kumshukuru Mugu kwa makuu aliyowatedea na ambayo alilitendea Jimbo kuu la Kigoma ambalo waliliongoza kwa awamu tofauti.

“Tunayo furaha ya moyoni, mdomoni na usoni, tunawakaribisha nyumbani jimboni Kigoma, tunawakaribisha nyinyi pamoja na wote mlioambatana nao ili kumshuruku Mungu kwa makuu aliyowatendea na ambayo analilitendea na analitendea jimbo kuu la kigoma ambalo mmeliongoza kwa awamu tofauti” alieleza Padre Guzuye.

Kwa niaba ya waamini wote Samsoni Mkanga  muumini  kutoka kanisa katoliki Prokia ya mtakatifu Mukasa Nguruka amesema kuwa, wanayo furaha kubwa kwa tukio hilo la Kihistoria kwani ni heshima kwa jimbo katoliki Kigoma ambapo amewaomba waamini wajitokeze kwa wingi hapo kesho kwa ajili ya Misa takatifu itakayo adhimishwa kwa ajili ya tukio hilo kubwa jimboni Kigoma.

Post a Comment

0 Comments