MKURUGENZI WA KUWASA AAHIDI KUBORESHA HUDUMA YA MAJI MANISPAA YA KIGOMA UJIJI



Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA),  Poas Kilangi  amewaahidi wananchi wa Manispaa ya Kigoma ujiji kuwa amedhamilia kuendelea kuboresha huduma za maji kwa Manispaa hiyo.

Kilangi ametoka ahadi hiyo wakati  wa kikao cha viongozi na wananchi wa mtaa wa Masanga uliopo katika Manispaa hiyo mkoani humo.

Kilangi ametoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kulipia ankara zao kwa wakati ili kazi ya usambazaji maji iwe nyepesi kwa maendeleo ya mkoa wa Kigoma.

Akifungua kikao hicho, Mhe. Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini Sharon Joseph amesema kuwa anayo imani na  utendaji kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA na watumishi wake ambapo amewasihi wananchi wa mtaa wa Msanga kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji katika mtaa huo itatatuliwa kwa manufaa yao.

"Watendaji wa KUWASA wapo kazini kutatua changamoto ya maji Masanga, nami nina imani nao" amesema Joseph.

Kwa niaba ya wananchi Chukilizo Emmanuel na Alfan Sudi, wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kupata huduma ya maji hasa wakati wa mchana ili kupunguza usumbufu wa kuchota maji usiku.

Post a Comment

0 Comments