JKCI YAANZA KUTOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGOMA

Na Emmanuel Matinde, Kigoma.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI kupitia huduma ya tiba mkoba iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka kambi ya siku tatu mkoani Kigoma kwa ajili kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto na watu wazima pamoja na kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na magonjwa hayo.

Akitoa taarifa ya kambi hiyo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dr. Eva Wakuganda, amesema tatizo la magonjwa ya moyo ni kubwa hapa nchini ambapo tangu kuanza kwa mfuko wa tiba mkoba chini ya Rais Samia asilimia 40% ya watu elfu 11,254 waliofikiwa wamebainika kuwa na magonjwa hayo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Kitabibu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni Dr. Bonipace Kilangi amesema kulingana na takwimu za hospitali za robo ya tatu ya mwaka magonjwa ya moyo pamoja na shinikizo la damu ni namba mbili baada ya magonjwa upasuaji.

Baadhi ya wananchi waliofika kunufaika na huduma hiyo walikuwa na haya ya kusema.

Zaidi ya watu mia tatu wanatarajiwa kuonwa na madaktari bingwa katika kambi hiyo mkoani Kigoma.


Post a Comment

0 Comments